Ufuatao ni mhutasari wa matukio yaliyogonga vichwa vya habari kama tulivyo yapokea katika chumba chetu cha habari leo.
Mgonjwa ajitia kitanzi hospitalini Vihiga
Hospitali kuu ya Vihiga imegonga vichwa vya habari siku za hivi karibuni kutokana na huduma duni ya matibabu katika hospitali hiyo na mapema hivi leo mgonjwa mmoja amejitia kitanzi katika hospitali hiyo kwa sababu zisizo julikana.
Bodaboda Likuyani watakiwa kuwa makini kuepuka visa vya kuvamiwa
Chifu wa kata ya likuyani, kaunti ya Kakamega Charles Banda, amewataka wahudumu wa boda boda katika sehemu hiyo kuupa usalama wao kipaumbele huku akisikitikia ongezeko la visa vya wahudumu hao kuvamiwa na kupokonywa pikipiki zao kando na kujeruhiwa.
Wakenya waombwa kuchagua viongozi faafu
Wito umetolewa kwa Wakenya kuwachagua viongozi kulingana a utendakazi wala sio kwa mirengo ya kisiasa.
Panpaper kuwapa zaidi ya 1500 ajira
Kufufuliwa kwa kiwanda cha panpaper kutatoa zaidi ya 1500 ya ajira kwa vijana katika eneo la magharibi na kuinua uchumi wa eneo hilo hasa mji wa Webuye ambao uchumi wake uliathirika pakubwa baada ya kufungwa kwa kiwanda hicho mwaka wa 2009.
Rais Uhuru Kenyatta alitangaza kufufuliwa tena kwa kiwanda cha pap paper kilichoko mjini webuye kwa muda wa miezi mitatu ijayo.
Rais alisema kuna mwekezaji ambaye tayari amenunua kiwanda hicho ameagiza kuwekeza takribani shilling billion 6.
Aidha rais alisema kwamba mwekezaji huyo atawapa kipaumbele wafanyakazi waliokuwepo kwenye kampuni hiyo kabla ya kiwanda hicho kushindwa kufanya shughuli zake.
Serikali ya Bungoma yaombwa kuajiri walimu wa chekechea zaidi
Serikali ya kaunti ya Bungoma, imetakiwa kuzidi kuajiri walimu zaidi wa shule za chekechea kuwezesha idadi kubwa ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo vya anwai kusomea taaluma hivyo kupata nafasi za ajira.
Kimataifa
Marekani imeitaka Urusi kuishinikiza Syria kusitisha kuvamia raia na badala yake kuzingatia makubaliano ya kusitisha mapigano.
Kwa kina cha habari hizi na zinginezo sikiliza West Fm katika masafa ya 94.9 na 104.1, au katika mtandao kwenye www.westfm.co.ke. Tegea runinga yetu ya West TV katika masafa ya Startimes 118 na Go Tv 805.