Ufuatao ni mhutasari wa matukio yaliyogonga vichwa vya habari kama tulivyo yapokea katika chumba chetu cha habari leo.
Shule ya upili ya wavulana ya Khasoko inakadiria hasara kubwa baada ya wanafuzi kugoma usiku wa kuamkia leo na kuharibu vifaa shuleni humo ikiwemo kupasua madirisha ya madarasa na vilevile kuharibu vifaa vya kielektroniki.
Ni mara ya pili sasa kwa wanafunzi wa shule hiyo kuandaa mgomo huku wakimtaka mwalimu mkuu david mwaturo kupewa uhamisho kwa kushindwa kuwashughulikia vyema na shule hiyo kutoandikisha matokeo mema.
Kaka wamfunga nduguyao mtini na kumpiga hadi kufa
Polisi mjini Kakamega wanawazuilia kaka wawili wanaokisiwa kumfunga ndugu yao kwa mti na kisha kumpiga hadi kufa kwa madai kuwa marehemu alisababisha baba yao kukamatwa.
Watoto nchini kupata chanjo ya Ukambi na Rubella
Takribani watoto elfu mia tisa na thelathini walio kati ya umri wa miezi 9 hadi miaka 14 wanatazamiwa kupokea chanjo dhidi ya ukambi katika kaunti ya kakamega kwenye zoezi la siku tisa lililong’oa nanga kote nchini jumatatu hii.
Serikali yatakiwa kuhakikisha zahanati zina wauguzi
Wito umetolewa kwa serikali ya kaunti ya Bungoma kuhakikisha zahanati na hospitali zote zinapokea dawa na wauguzi wa kutosha kama njia moja ya kuzuia vifo ambavyo vinaendelea kushudiwa.
Kimataifa
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye anahamishwa kutoka gereza la Moroto kaskazini mashariki mwa nchi kwenda gereza la Luzira lililo mji mkuu Kampala ambalo ndilo gereza kubwa zaidi nchini humo.
Kwa kina cha habari hizi sikiliza West Fm katika masafa ya 94.9 na 104.1, au katika mtandao kwenye www.westfm.co.ke. Tegea runinga yetu ya West TV katika masafa ya Startimes 118 na Go Tv 805.