Ufuatao ni mhutasari wa matukio yaliyogonga vichwa vya habari kama tulivyo yapokea katika chumba chetu cha habari leo.
Raisi aahidi kufunguwa kiwanda cha Pan Paper
Rais Uhuru Kenyatta ameahidi kuwa serikali yake inaenda kufufua kiwanda cha karatasi cha Pan Paper mjini Webuye kwa muda wa miezi mitatu ijayo ili kuimarisha uchumi wa kaunti ya Bungoma na nchi hii kwa ujumla
Akihutubu katika ikulu ya Nairobi rais amesema kuwa kuporoka kwa kiwanda hicho kulirudisha nyuma maendeleo eneo la Webuye na eneo la magharibi huku idadi kubwa ya watu ikikosa ajira
Wakimbizi wa ndani kwa ndani Vihiga hawajafidiwa-gavana

Gavana wa kaunti ya vihiga Moses Akaranga anasema kuna wakimbizi wa ndani kwa ndani katika eneo hilo ambao walipoteza mali yao baada ya ghasia za uchaguzi wa mwaka wa elfu mbili na kumi na saba na hadi sasa hawaja fidiwa na serikali.
Kizaazaa Likuyani, mkaazi afumaniwa na mke wa jirani
Kulizika kizaazaa katika kijiji cha Mutembei kata ya Kongoni kaunti ndogo ya Likuyani, baada ya mzee wa mtaa huo Geofrey Wafula Simiyu kufumaniwa akila uroda na jiraniye wakike.
Gavana wa Nandi azindua miradi ya maji
Gavana wa kaunti ya Nandi daktari Cleophas Lagat, ameandaa misururu ya mikutano katika wadi ya Kaptel/Kamoiywo kwenye eneo bunge la Chesumei kuzindua rasmi miradi mbalimbali ya maji kwa wenyeji wa eneo hilo.
Mradi wa kusambaza stima wazinduliwa Butere
Maelfu ya wakaazi wilayani Butere wana kila sababu ya kutabasamu, baada ya mfanyi biashara mmoja kutoka eneo hilo Tindi Mwale, kuzindua mradi wa kusambaza stima kwa zaidi ya nyumba elfu nne.
Mshukiwa wa utapeli atiwa mbaroni Webuye mashariki
Maafisa wa polisi mjini Webuye wamemtia mbaroni mwanamume mmoja anayeshukiwa kuwa miongoni mwa kundi la watu wanaowatapeli wakaazi hela zao.
Kwa kina cha habari hizi na zinginezo sikiliza West Fm katika masafa ya 94.9 na 104.1, au katika mtandao kwenye www.westfm.co.ke. Tegea runinga yetu ya West TV katika masafa yaStartimes 118 na Go Tv 805.