Ufuatao ni mhutasari wa matukio yaliyogonga vichwa vya habari kama tulivyo yapokea katika chumba chetu cha habari leo.
Kampeni ya kupeana chanjo ili kuzuia ugonjwa wa ukambi na Rubella imeendelea kwa siku ya pili katika kaunti ya Trans Nzoia huku idadi kubwa ya watoto ikipewa chanjo hiyo katika vituo tofauti.
Kwa mujibu wa kaimu mwanachama wa mamlaka ya kaunti kitengo cha afya Isaac Kogo wanalenga kutoa chanjo hiyo kwa asilimia 43 ya watoto katika kaunti hii
Serikali ya Bungoma yapewa ilani kukarabati soko la Chwele
Mwakilishi wa wadi ya Chwele Kabuchai James Mukhongo ametoa ilani ya siku 21 kwa serikali ya kaunti ya Bungoma kukarabati soko la Chwele la sivyo wafanyibiashara wasusiye kutowa ushuru.
Wakaazi Mumias wapata hasara kutokana na Kiboko
Wakaazi wa kijiji cha Butobe eneo bunge la Mumias magharibi wanaendelea kukadiria hasara ya mimea yao inayoharibiwa na Kiboko ambaye pia huwaangaisha nyumbani kwao kila mara.
Wakiongozwa na Francis Omengo wakaazi hao wanasema kuwa mimea yao imekuwa ikiaribiwa na Kiboko huyo kwa muda mrefu huku maisha yao yakisalia kuwa hatarini.
Mahakama yashutumiwa kuzua chuki miongoni mwa wakaazi Busia
Gavana wa kaunti ya Busia Sospeter Ojaamong na mwakilishi wa wadi ya Nangina John Obwogo wameyashutumu mahakama kwa kuzua uhasama katika kaunti ya Busia kwa kufunga viwanda viwili vya sukari.
Wawili hao wamesema hatua hiyo ya mahakama iimesababisha uhasama kati ya jamii ya Waluhya na Wateso mbali na kulemaza maendeleo.
Wakaazi shinyalu waombwa kuchukua vitambulisho
Wakaazi wa eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega ambao walijiandikisha kupata vitambulisho vya kitaifa wametakiwa kutembelea afisi za usajili pamoja na afisi za utawala katika maeneo yao, ili wachukue stakabadhi hizo muhimu.
Kwa kina cha habari hizi sikiliza West Fm katika masafa ya 94.9 na 104.1, au katika mtandao kwenye www.westfm.co.ke. Tegea runinga yetu ya West TV katika masafa ya Startimes 118 na Go Tv 805.