Raisi Uhuru Kenyatta amemteua aliyekuwa mbunge wa Bumula Bifwoli Wakoli kuwa mwenyeketi wa shirika la Ukulima na maendeleo yaani Agricultural Development Corporation Board.
Bifwoli ameteuliwa kuchukua mahali pa aliyekua mbunge wa Malava Soita Shitanda aliyefariki mwezi jana akiwa mwenyekiti wa shirika hilo na kuacha pengo hilo.
Bifwoli atashikilia nafasi hiyo kwa muda wa miaka mitatu kuanzia Alhamisi tarehe 24 Juni 2016.
Mwanawe Masinde Muliro, Mwambu Muliro ateuliwa mwenyekiti wa Kenya Utalii
Mwanawe aliyekuwa mwanasiasa maarufu magharibi ya Kenya hayati Masinde Muliro, Mwambu Muliro ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa Kenya Utalii.
Uteuzi wa Mwambu unajiri takribani mwaka mmoja tangu kifo cha mkewe hayati Masinde Muliro.
Katika mazishi ya mkewe marehemu Masinde mwaka 2015, Waziri wa Maji na Unyunyuziaji mashamba maji Eugine Wamalwa aliwaahidi waombolezaji na jamaa kuwa familia ya kigogo huyo ilikuwa kwenye mpango wa serikali ya Jubilee na wakati wowote ingekumbukwa kutokana na mchango mkubwa wa marehemu nchini.
Nandi yazindua mbinu ya kukusanya ushuru kielektroniki
Serikali ya kaunti ya Nandi imezindua teknolojia mpya ya kisasa ya ukusanyaji ushuru ya e -nandi iliyobuniwa kutoka taifa la Uganda.
Teknologia hii inahusishwa ukusanyaji wa ushuru katika njia ya kidijitali.
Kaunti ya Nandi itakuwa miongoni mwa kaunti zingine ambazo zimepokea mbinu ya ukusanyaji ushuru kielektroniki ikiwemo Bungoma, Nairobi, Kisumu, Machakos, Nakuru na Kiambu.
Bodaboda waandamana Kapenguria
Mamia ya wahudumu wa bodaboda mjini Kapenguria hapo jana waliandaa maandamano kulalamikia hatua ya kunyanyaswa na maafisa wa polisi.
Wahudumu hao walishurutisha kuachiliwa huru kwa wenzao wawili waliotiwa mbaroni kwa kushukiwa kumpiga mwanaume mmoja aliyehusika katika ajali, wakiwashtumu maafisa wa polisi kwa kutomkamata aliyesababisha ajali iliyomwacha abiria mmoja ameaga huku mhudumu wa boda boda akijeruhiwa
Afisa anayesimamia kituo cha polisi cha Kapenguria Vitalis Ochido na kamanda wa polisi Pokot magharibi waliwahakikishia waandamanaji hao kuwa mshukiwa aliyesababisha ajali hiyo atatiwa mbaroni .
Oparanya asisitiza kujitolea kwake kushirikiana na viongozi wengineKakamega
Gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Ambetsa Oparanya ameelezea kujitolea kwake kushirikiana na viongozi wote waliochaghuliwa na wakaazi wa kaunti hiyo bila kuangalia mirengo ya kisiasa ili kuafiki maendeleo kwa wakaazi wa kaunti hiyo.
Gavana huyo alihoji kuwa kama gavana hana mapendeleo yoyote na kuahidi kushirikiana vilivyo na viongozi waliochaghuliwa na wakaazi wakaunti hiyo bila ubaguzi wa mirengo ya kisiasa.
Wakulima washauriwa kushiriki katika ufugaji wa sungura
Wakulima katika kaunti ya bungoma wameshauriwa kushiriki kwa kina katika kilimo cha ufugaji wa sungura ili kujiinua kiiuchumi na kimaisha.
Metrine Makokha ambaye ni mmoja wa wakulima wanaoendeleza ufugaji wa sungura asema kuwa kilimo hicho kinahitaji sehemu ndogo na ni rahisi kuwalisha ikizingatiwa kuwa wanategemea magugu ya shamba.
Aliongezea kuwa sungura hukoma baada ya miezi tisa na soko lake hupatikana kwa urahisi kufuatia idadi kubwa ya watu wanaokula nyama hio