Cord waandamana kubandua IEBC mamlakani
Yafuatayo ni matukio yaliyogonga vichwa vya habari kama tulivyo yapokea katika chumba chetu cha habari leo jioni.
Cord waandamana kubandua IEBC mamlakani
Viongozi wa mrengo wa upinzani nchini (Cord) wamekabiliwa na maafisa wa usalama baada yao kuandamana hadi makao makuu ya tume ya uchaguzi (iebc) wakitaka ing’atuke mamlakani.
Maji safi kwa shule za umma maeneo kame
Wizara ya Maji na Unyunyuziaji Mashamba Maji inalenga kuhakikisha kuwa shule zote za umma zilizoko katika maeneo kame zinapata huduma za maji safi.
Waziri Eugine Wamalwa anasema wizara yake i mbiyoni kuhakikisha kuwa shule za umma zinakuwa na maji safi ya matumizi.
Serikali yazindua ruwaza kukabili ukame Pokot
Serikali imezindua ruwaza ya mwaka 2022 ya kukakabili athari za makali ya ukame katika kaunti ya Pokot magharibi huku eneo hilo likisalia mojawapo ya maeneo nchini yanayoathirika pakubwa na ukame.
Huduma za CDF Mlima Elgoni kutatizika
Huenda wakaazi katika eneo bunge la Mlima Elgon wakazidi kusubiri kwa muda usiojulikana kupata huduma za hazina ya CDF baada ya kundi moja kufika mahakamani kupinga kuteuliwa kwa kamati ya hazina hiyo yenye uwezo wa kutekeleza miradi inayopitishwa.
Spika wa Vihiga Dan Chitwa aanza kuchunguzwa rasmi
Kamati ya bunge katika bunge la kaunti ya Vihiga iliyo buniwa kumchunguza spika wa bunge hilo Dan Chitwa imeanza rasmi vikao vya kumuchunguza spika huyo kutokana na utumizi mbaya wa fedha na mamlaka katika bunge hilo.
Familia yalilia haki ya mwanao alinajisiwa
Familia moja kutoka kijiji cha Bushiri kata ya Ingotse eneo bunge la Navakholo kaunti ya Kakamega inaomba mashirika ya kutetea haki za watoto kuingilia kati na kuhakikisha kuwa mzee aliyemnajisi mwanao wa miaka 10 anachukuliwa hatua kali za kisheria.
Mzozo kati ya wafanyibiashara na serikali wanukia Kitale
Mzozo unatokota kati ya wafanyibiashara mjini Kitale katika eneo la Chanuka na serikali ya kaunti ya Trans Nzoia baada ya kubainika kuwa kipande cha ardhi cha wafanyibiashara hao ambacho wamekuwa wakifanyia biashara kimeuzwa.
Ugonjwa wa Malaria wabakia kero Busia na Bungoma
Asilimia arobaini ya wakaazi wa kaunti ya Busia huugua ugonjwa wa malaria kila mwaka.
Huku taifa la Kenya likijiunga na mataifa mengine ulimwenguni kuadimisha Siku ya Malaria Duniani, ugonjwa wa malaria umetajwa kuwa tishio kwa maisha ya mama mja mzito katika kaunti ya Bungoma.
Bensouda aanza uchunguzi wa awali kuhusu mauaji Burundi
Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) amesema mahakama hiyo imeanzisha uchunguzi wa awali kuhusu mauaji ambayo yamekuwa yakitokea nchini Burundi.
Bi. Fatou Bensouda amesema amekuwa akifuatilia kwa karibu matukio Burundi tangu Aprili 2015 na kwamba mara kwa mara amezitaka pande zote husika kutojihusisha na ghasia na amauaji.
Kwa kina cha habari hizi sikiliza West Fm katika masafa ya 94.9 na 104.1, au katika mtandao kwenye www.westfm.co.ke. Tegea runinga yetu ya West TV katika masafa yaStartimes 118 na Go Tv 805.