Yafuatayo ni matukio yaliyogonga vichwa vya habari kama tulivyo yapokea katika chumba chetu cha habari leo.
Askofu mkuu wa kanisa la Kiangilikana nchini Eliud Wabukala anaendelea kupokea ujumbe wa heri jema kutokana na kazi nzuri aliyoitekeleza akiwa kiongozi wa kanisa hilo mbele ya muda wake wa kustaafu kukamilika.
Askofu huyo ambaye anastaafu Juni 26 mwaka huu atakumbukwa kwa msimamo wake dhabiti wa kuikosoa serikali na kuwatetea wanyonge ili wapate haki zao.
Gavana adai wanaotilia shaka uongozi wake wana chuki
Gavana wa kaunti ya Busia Sospeter Odeke Ojaamong amewasuta vikali baadhi ya viongozi wanaotilia shaka uongozi wake na kudai kuwa wanaongozwa na chuki ya kisiasa na kikabila.
Haya yanajiri siku chache tu baada ya mbunge wa Budalangi Ababu Namwamba na mwenzake wa Teso kaskazini Arthur Odera kumshutumu gavana huyo kwa kukosa kuafiki miradi mingi ya maendeleo katika kaunti ya Busia.
Chama chataka wauguzi kutengewa pesa ya kujiongeza masomo
Chama cha wauguzi nchini kimetoa wito kwa magavana kutenga kiasi fulani cha fedha katika bajeti zao kwa minajili ya kuwafadhili wauguzi ambao wana azmio la kuendeleza masomo yao kwenye taaluma hiyo.
Serikali yaraiwa kuweka matuta barabarani kuepusha ajali
Serikali ya kaunti ya Bungoma na ile ya kitaifa zimetakiwa kushirikiana katika shughuli ya kuweka matuta na kuzibwa kwa mashimo kwenye barabara kuu ya Kimilili-Bokoli-Sikata kuzuia uwezekano wa kuzuka kwa ajali za barabarani.
Uchaguzi Mumias Sugar wakamilika vyema
Uchaguzi wa viongozi katika idara mbalimbali kwenye kiwanda cha Sukari cha Mumias umekamilika vyema bila vurugu kama ilivyokuwa imetarajiwa hapo awali.
Wakaazi Matungu watakiwa kukumbatia elimu ya mtoto wa kike
Wakaazi wilayani Matungu, kaunti ya Kakamega wametakiwa kukumbatia elimu ya mtoto wa kike ili kuiendeleza jamii yenye maono mema.
Wakaazi wa Bungoma waonywa dhidi ya bombe haramu
Tahadhari imetolewa kwa wakaazi wa Bungoma kujiepusha na biashara ya pombe haramu katika taifa jirani la Uganda baada ya kugundua kuwa ulanguzi huo wa pombe haramu umezidi kwa kiwango cha juu
Kwa kina cha habari hizi sikiliza West Fm katika masafa ya 94.9 na 104.1, au katika mtandao kwenye www.westfm.co.ke. Tegea runinga yetu ya West TV katika masafa ya Startimes 118 na Go Tv 805.