Ufuatao ni mhutasari wa matukio yaliyogonga vichwa vya habari kama tulivyo yapokea katika chumba chetu cha habari leo.
Jubilee yakashifu maandamano ya Cord
Viongozi wanaoegea mrengo wa jubilee wamekashifu vikali hatua ya wanacord kuandamana hadi afisi za tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka kutaka kuwatimu makamishona wa tume hiyo.
Shrika la Fanisi lajitolea kuimarisha kilimo Likuyani
Shirika lisilokuwa la kiserikali la Fanisi, limeratibu kuwatafuta waekezaji na wataalamu wa kilimo kutoka mataifa ya ughaibuni ili kusaidia kuimarisha sekta ya kilimo katika kaunti ndogo ya likuyani.
“Ungeni azma ya Wetangula ya uraisi,” mbunge asema
Mbunge wa kimilili Suleiman Kasuti Murunga, ametoa wito kwa viongozi kutoka eneo la magharibi, kuunga mkono azma ya seneta wa kaunti ya bungoma Moses Wetangula ya kuwa rais akisema ana tajriba kuu ya kuongoza nchi hii.
Vijana Bungoma waraiwa kutokubali kutumiwa na wanasiasa
Kiongozi wa baraza la kitaifa la vijana katika kaunti ya Bungoma, Moses Wanyama, amewataka vijana kutotumiwa na wanasiasa kuvuruga mikutano ya hadhara na badala yake kujishughulisha na masuala ya maendeleo

Wito wa amani na uwiano watolewa mbele ya uchaguzi mkuu ujao
Mwakilishi wa wadi ya Sikhendu Andrew Sichangi Kutilila ametoa wito wa amani na uwiano mbele ya uchaguzi mkuu ujao akisema serikaki inastahili kutatua masaibu yanayowakumba wakenya kwa wakati ufaao.
Kura ya kuchagua wagombea uraisi kupigwa marekani
Wapiga kura katika majimbo matano kaskazini mashariki ya marekani watapiga kura katika uchaguzi wa mchujo wa kuteua wagombea wa vyama vya republican na democratic.
Kwa kina cha habari hizi sikiliza West Fm katika masafa ya 94.9 na 104.1, au katika mtandao kwenye www.westfm.co.ke. Tegea runinga yetu ya West TV katika masafa yaStartimes 118 na Go Tv 805.