Ufuatao ni mhtasari wa matukio kama tulivyo yapokea katika chumba chetu cha habari leo 10/06/2016.
Mama wa taifa Bi. Margaret Kenyatta ametoa wito kwa viongozi nchini kuunga mkono vita dhidi ya ugonjwa wa ukimwi na maradhi mengine nchini.
Akihutubu katika shule ya msingi ya Grace Compasion Mundika katika sherehe ya kukabidhi kaunti ya Busia kliniki tamba, mama wa taifa ameelezea kujitolea kwake kuhakikisha kuwa akina mama hasa wajawazito wanapata huduma bora ya afya.
Kiwanda cha Panpaper kufunguliwa rasmi Agosti
Wananchi kutoka maeneo bunge ya Webuye mashariki na magharibi hii leo walihusisha katika majadiliano kuhusu mazingira huku kiwanda cha kutengeza karatasi cha Panpaper mjini Webuye kinapotarajiwa kufunguliwa rasmi mwezi wa nane.
Kiwanda cha samaki Kakamega kuanza kazi baada ya wiki 2
Kiwanda cha kutayarisha bidhaa za samaki kilichojengwa mjini Kakamega kwa gharama ya shilingi milioni sabini kinatarajiwa kuanza oparesheni kwa muda wa majuma mawili yajayo baada ya kusubiriwa kwa muda.
Wanafunzi 3 walazwa baada ya kugongwa na gari la wagonjwa
Wanafunzi watatu wa shule ya msingi ya mtakatifu Francis Majengo katika kaunti ndogo ya Lugari wamelazwa katika hospitali kuu ya sehemu hiyo baada ya kugongwa na ambulance ya hospitali ya kibinafsi ya Chebaiywa walipokuwa wakielekea nyumbani kwa chakula cha mchana hii leo.
Polisi wazuiliwa kwa tuhuma za mauaji Mumias
Polisi wawili wa utawala wametiwa nguvuni na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha mumias kwa tuhuma za mauaji ya mwanamme mmoja katika eneo la Lunganyiro
Mwanamme afa baada ya kujiteketeza
Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 40 ameripotiwa kufariki baada ya
kujifungia ndani ya nyumba na kujiteketeza
Kimataifa
Wapiganaji wa kundi la al-shabab nchini Somalia wanasema kuwa wamewaua wanajeshi 40 wa Ethiopia katika kambi ya umoja wa Afrika katikati ya Somalia.
Wanamgambo wa Islamic State wameendesha mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga ndani na nje ya mji wa Iraq, Baghdad ambapo takriban watu 30 wameuawa.
Kwa kina cha habari hizi sikiliza West Fm katika masafa ya 94.9 na 104.1, au katika mtandao kwenye www.westfm.co.ke. Tegea runinga yetu ya West TV katika masafa ya Startimes 118 na Go Tv 805.