Yafuatayo ni matukio yaliyogonga vichwa vya habari kama tulivyo yapokea katika chumba chetu cha habari leo jioni.
Msafara wa Safaricom mtaani wazuru Bungoma
Msafara wa Safaricom mtaani ijumaa hii umezuru baadhi ya maeneo katika kaunti ya Bungoma huku wengi wa wenyeji waliojitokeza wakituzwa na kupata mafunzo muhimu hasa ya kuepuka kulaghaiwa..
Wanawake waraiwa kuwania nyadhifa za uongozi nchini
Mbunge wa kaunti ya Trans Nzoia Bi. Janet Nangabo amewasihi akinamama kutokufa moyo baada ya mswada wa kijinsia kutopata uungwaji mkono hapo jana kwenye bunge la kitaifa na kuwarai kuwania nyadhifa mbali mbali za uongozi
Wanabodaboda watakiwa kupata mafunzo ya kuendesha pikipiki
Wito umetolewa kwa wahudumu wa bodaboda aina ya pikipiki kutafuta mafunzo ya kuendesha pikipiki barabarani ili kuzuia vifo vya ajali vinavyotokana na uendeshaji mbaya wa pikipiki.
Kiwanda cha kuchinjia kuku kuanza kazi baada ya wiki mbili
Gavana wa Kaunti ya Bungoma Kenneth Lusaka amewahakikishia wakaazi wa kaunti ya Bungoma kwamba kiwanda cha Chwele cha kuchinja kuku kitaanza kufanya kazi baada ya wiki mbili.
Kimataifa
Serikali ya Uganda inafanya utathmini ambao huenda ukapelekea kutolewa kwa majeshi ya nchi hiyo nchini Somalia na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Spika wa Republican katika baraza la wawakilishi la Marekani, Paul Ryan, amesema hayupo tayari kumuunga mkono Donald Trump kuwa mgombea wa urais kupitia chama hicho.
Kwa kina cha habari hizi sikiliza West Fm katika masafa ya 94.9 na 104.1, au katika mtandao kwenye www.westfm.co.ke. Tegea runinga yetu ya West TV katika masafa ya Startimes 118 na Go Tv 805.