Yafuatayo ni matukio yaliyogonga vichwa vya habari kama tulivyo yapokea katika chumba chetu cha habari leo.
Katibu mkuu wa shule za kibnafsi eneo bunge la Navakholo Rodgers Nato amewahimiza wakurugenzi na wamiliki wa shule za kibnasfi eneo hilo kujizatiti ili kuakikisha kuwa wanafunzi wao wanapata vipatakilishili ili kuwiana na ule mpango wa serikali wa kutoa vipatakilishi kwa wanafunzi wa darasa la kwanza kote nchini.
Mwili wa mwanaume wapatikana ukining’inia mtini
Hali ya huzuni imetanda katika kijiji cha Vilongo kata ya Mautuma kaunti ndogo ya Lugari baada ya mwili wa mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 38 kupatikana ukining’inia mtini shambani mwa jiraniye alfajiri ya leo.
Viongozi wa kidini Busia wawaonya wanasiasa dhidi ya ukabila
Huku joto la kisiasa zinazoegemea ukabila likiendelea kupanda katika kaunti ya Busia, viongozi wa kidini kutoka kaunti hiyo wamewasihi wanasiasa kujiepusha na ukabila.
Wenyeji Sichei waonywa kuhusisha wanavunzi katika pombe
Chifu wa kata ndogo ya Sichei eneo bunge la Kabuchai John Mwanja amewaonya wenyeji wa eneo hilo kukoma kuwahusisha watoto wa shule na ugemaji wa pombe haramu kabla hawajakumbana na makali ya sheria.
Kina mama Nandi wahimizwa kufanya kazi ya mikono
Kina mama katika kaunti ya Nandi wasio na ajira wametakiwa kujitokeza kwa wingi na kutumia kikamilifu kazi ya mikono yao kujiendeleza katika maisha yao ya kila siku.
Wakaazi Mumias wachimbiwa visima na mhisani
Ni afueni sasa kwa wakaazi wa kijiji cha Khungwani eneo bunge la Mumias baada ya kukumbwa na magonjwa tofauti kutokana na maji chafu waliokuwa wakinywa baada ya kuchimbiwa kisima na muhisani wa eneo hilo
Kimataifa
Jeshi la marekani limesema mmoja wa viongozi wakuu wa kundi linalojiita Islamic State ameuawa kwenye shambulizi la kutoka angani.
Msemaji wa Pentagon Peter Cook amesema Abu Waheeb, ambaye amekuwa afisa mkuu wa kijeshi wa Islamic State katika mkoa wa Anbar nchini Iiraq aliuawa pamoja na watu wengine watatu baada ya gari lao kushambuliwa katika eneo la Rutba.
Mgombea urais wa chama cha Republican nchini marekani Donald Trump amesema meya mpya wa jiji la London ambaye ni mwislamu hangezuiwa kuzuru marekani iwapo pendekezo lake kwamba waislamu wazuiwe kwa muda kuingia marekani lingetekelezwa.
Kwa sababu ya imani yake, meya huyo mpya Sadiq Khan amesema ana shaka kuhusu iwapo ataruhusiwa kuzuru marekani iwapo Bw. Trump atachaguliwa kuwa rais.
Kwa kina cha habari hizi sikiliza West Fm katika masafa ya 94.9 na 104.1, au katika mtandao kwenye www.westfm.co.ke. Tegea runinga yetu ya West TV katika masafa ya Startimes 118 na Go Tv 805.