Viongozi Bonde la Ufa kushitaki Uingereza
Kila siku, www.westfm.co.ke inakuletea kwa muhtasari matukio muhimu kutoka katika maeneo ya Magharibi ya nchi ya Kenya na dunia yote kwa ujumla ili ukapate kujua kwa upana na utendeti ulimwengu ulivyo.
Yafuatayo ni matukio yaliyogonga vichwa vya habari kama tulivyo yapokea katika chumba chetu cha habari leo.
- Viongozi kutoka Bonde la Ufa kushitaki serikali ya Uingereza
Viongozi kutoka kanda ya kaskazini ya Bonde la Ufa wametishia kuishtaki serikali ya Uingereza kwa dhuluma za kihistoria zilizofanyiwa wafuasi wa Dini ya Roho ya Mafuta ya Pole Afrika, ili kuhakikisha wanapata haki kama wapiganaji wa uhuru.
2. Kaunti ya Bungoma yatakiwa kuboresha huduma hospitalini
Serikali ya kaunti ya Bungoma imetakiwa kuangazia kwa kina kuboresha huduma katika hospitali za umma ili kuwezesha wakaazi kutosafiri mwendo mrefu kutafuta huduma za matibabu.
3. KNUT tawi la Lugari yawataka wanachama kudhibitisha uanachama
Naibu katibu mkuu wa chama cha kutetea masilahi ya walimu KNUT tawi la Lugari Nahashon Wambulwa, amewataka walimu wa eneo hilo kuthibitisha uanachama wao katika muungano huo hasa baada ya tume ya kuwaajiri walimu nchini TSC kudaiwa kuuvuruga uanacha wa muungano huo.
4. Serikali ya Kaunti ya Nandi yalaumiwa kushindwa kutekeleza wajibu wake
Serikali ya kaunti ya Nandi imelaumiwa pakubwa kwa kufeli kutekeleza wajibu wake licha ya kuwa uongozini kwa kipindi cha miaka mitatu sasa hali ambayo imewaacha wenyeji wa nandi na masaibu chungu nzima
5. Wapinzani wafanya mipango kumng’amua Donald Trump katika kinyang’anyiro cha urais Marekani
Wapinzani wawili wakuu wa Donald Trump katika kinyang’anyiro cha kumteua mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani, wametangaza mipango ya kuungana kukabiliana na mgombea huyo. Ted Cruz na John Kasich wanataka kushirikiana kupunguza uwezekano wa mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York kushinda mchujo katika majimbo zaidi.
Kwa kina cha habari hizi sikiliza West Fm katika masafa ya 94.9 na 104.1, au katika mtandao kwenye www.westfm.co.ke. Tegea runinga yetu ya West TV katika masafa ya Startimes 118 na Go Tv 805.