Kila siku, www.westfm.co.ke inakuletea kwa muhtasari matukio muhimu yanayogonga vichwa vya habari ili upate kujua yaliyotendeka ndani na nje ya nchini kwa urahisi. Haya ndiyo matukio tuliyoyapa uzito siku ya Jumanne, Mei 31.
Viwango vya masomo vyadidimia Sirisia
Wito umetolewa kwa washika dau mbalimbali katika sekta ya elimu kwenye kaunti ndogo ya Sirisia kushirikiana kikamilifu ili kuboresha viwango vya masomo ambavyo vinaendelea kudidimia.
Wakaazi Sabatia wapinga kuhamiswa kwa shule ya Vokoli
Baadhi ya viongozi katika wadi ya Wodanga katika eneo bunge la Sabatia wakiongozwa na mwakilishi wa wadi hiyo Vincent Atsiaya wamepinga hatua ya kuhamishwa kwa shule ya wasichana ya Vokoli kutoa nafasi kwa kuanzishwa kwa chuo kikuu cha Vihiga cha Sayansi na Teknolojia.
Muungano wa wauguzi wapinga uhamisho wa wauguzi Kakamega
Muungano wa wauguzi katika kaunti ya Kakamega umepinga pendekezo la serikali ya kaunti kuwapa uhamisho wa jumla wauguzi ambao wamehudumu katika vituo vya afya kwa zaidi ya miaka sita.
N.C.P.B yawapa waathriwa wa mafuriko Trans Nzoia msaada
Wakaazi wa eneo la Marinda katika kaunti ya Trans Nzoia ambao waliathirika na mafuriko kufuatia kuvunja kwa kingo ya mto Sabwani hii leo wamepata msaada wa mahindi kutoka shirika la bodi ya nafaka na mazao (N.C.P.B.).
Kimataifa
Takriban watu saba waliuwawa siku ya Jumatatu mashariki mwa mji wa Asaba, nchini Nigeria katika vita dhidi ya watu wa jamii ya Biafra wanaotaka kujitenga na jeshi la taifa hilo kulingana na shirika la habari la Associated Press.
WHO yatoa onyo dhidi ya virusi vya Zika, yawataka watu kumakinika
Shirika la afya dunia (WHO) linawahimiza watu wanaotoka katika sehemu zilizoathirika na virusi vya zika kuzingatia mbinu za kujikinga endapo mtu anafanya mapenzi ama kujiepusha na ngono kwa muda wa wiki nane.
WHO pia imeongeza kwamba wanawake waepukane na kupata mimba kwa miezi sita iwapo mwenzake wa ndoa amekuwa na dalili za virusi vya ugonjwa huo.