Ufuatao ni mhutasari wa matukio yaliyogonga vichwa vya habari kama tulivyo yapokea katika chumba chetu cha habari leo.
Wakaazi wa kaunti ya Bungoma walipata fursa ya kutazama filamu ya bure baada ya baadhi ya wananchi kujishikilia kwenye ndege iliyokuwa imebeba maiti ya mfanyibiashara Jacob Juma huku wakimlazimu rubani kutua katika uwanja wa ndege wa Bungoma kabla ya kupaa tena.
Raila adai Juma aliuwawa ili kunyamazisha ukweli
Kinara wa CORD Raila Odinga amesema kuwa Jacob Juma aliuawa kwa kufichua uozo ulioko serikalini nakuwaeleza wahusika kuwa hawatafaulu kunyamazisha ukweli.
Ojaamong awataka wabunge kufutalia serikali kuu kwa fenda za maendeleo
Gavana wa kaunti ya Busia Sospeter Ojaamong ametoa changamoto kwa wabunge kutoka kaunti ya Busia kufuatilia fedha za maendeleo kutoka serikali kuu ili zisaidie kaunti.
Kikao chafanyika kutatua utata wa mpaka Maseno
Kamati ya sheria katika bunge la kitaifa imeitembelea kaunti ya Vihiga na kuandaa vikao vya kuchukua maoni ya wakaazi wa eneo la Emuhaya katika shule ya msingi ya Ebusakami hivi leo kuhusiana na utata wa mpaka wa eneo la Maseno ambao umekuwepo kwa muda mrefu.
Wakazi Lugari watoa wito kutengenezewa daraja kwenye Mto Lumakanda
Wakaazi wa vijiji vya Mwivona katika wadi ya Lugari na Bondeni katika wametoa wito kwa viongozi wa sehemu hiyo kuwasaidia kujenga daraja kuziunganisha wadi hizo baada ya kivukio walichokuwa wakitegemea kuuvuka Mto Lumakanda kusombwa na maji kufuatia mvua kubwa inayonyesha katika sehemu hiyo.
Kimataifa
Ripoti ya siri ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa ilioonekana na shirika la habari la Reuters inaarifu kuwa maafisa kadhaa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamesema kuwa Korea kazkasini imewapatia wanajeshi na polisi bastola.
Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) imeonya kuwa hali ya uchafuzi wa hewa inazidi kuwa mbaya duniani kote huku zaidi ya asilimia 80 ya wakaazi wa miji mikubwa wakivuta hewa chafu na kuongeza hatari ya kupatwa na saratani ya mapafu na maradhi mengine hatari.
Kwa kina cha habari hizi sikiliza West Fm katika masafa ya 94.9 na 104.1, au katika mtandao kwenye www.westfm.co.ke. Tegea runinga yetu ya West TV katika masafa ya Startimes 118 na Go Tv 805.