Yafuatayo ni matukio yaliyogonga vichwa vya habari kama tulivyo yapokea katika chumba chetu cha habari leo.
Waziri wa Elimu Sayanzi na Technoligia Fred Matiangi ametoa agizo kwa mwalimu mkuu wa shule ya upili ya wasichana ya St. Marys Shihome kuhakikisha kwamba anawasajili wanafunzi ambao walipata uja uzito kwenye shule hiyo kuukalia mtihani wao wa kidato cha nne mwaka huu.
Haya yanajiri baada ya shule hiyo kuwakatalia mbali wasichana hao waliopata uja uzito kukalia mtihani wao mwaka huu.
Mshukiwa wa wizi avamiwa na wanakijiji
Mshukiwa mmoja wa wizi wa mifugo kutoka kijiji cha Ojamii eneo bunge la Teso kusini alilazimika kutimua mbio kuokoa maisha yake baada ya kuvamiwa na wanakijiji waliyomshuku kuhusika na uovu huo.
Viongozi Pokot wapinga maandamano ya CORD
Viongozi kutoka kaunti ya Pokot magharibi, wamepinga maandamano yanayoongozwa na mrengo wa upinzani CORD dhidi tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka IEBC, huku wakipendekeza wanacord kufuatia sheria katika mchakato wa kuiondoa tume hiyo.
Msichana aaga baada ya kuangukiwa na mti
Msichana mmoja mwenye umri wa miaka ishirini ambaye amekuwa akihudumu kama mfanyikazi wa nyumba katika eneo la Nandihils kaunti ya Nandi, ameripotiwa kufariki papo hapo baada ya kuangukiwa na mti uliokuwa ukikatwa.
Mama na mwanawe wazuiliwa kwa tuhuma za mauaji
Maafisa wa polisi katika kaunti ndogo ya Lugari wanamzuilia mama na mwanawe wa kiume kwa tuhuma za kumpiga na kumuua mvulana mmoja katika kijiji cha Jerusalem kata ya Mautuma.
Viongozi waraiwa kujenga hospitali Eluuya, Tongareni
Wito umetolewa kwa viongozi katika eneo bunge la Tongaren kujitokeza kusaidia ujenzi wa hospitali eneo la Eluuya ili kuleta huduma hiyo karibu kuwezesha wakaazi kutosafiri mwendo mrefu kutafuta huduma za matibabu kwingineko.
Kimataifa
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema kuwa serikali yake imepigwa na butwaa na matamshi ya kushtua na ya aibu ya waziri mkuu wa uingereza Bw. David Cameron yakwamba Nigeria na Afghanistan ndio mataifa fisadi zaidi duniani.
Kwa kina cha habari hizi sikiliza West Fm katika masafa ya 94.9 na 104.1, au katika mtandao kwenye www.westfm.co.ke. Tegea runinga yetu ya West TV katika masafa ya Startimes 118 na Go Tv 805.