Yafuatayo ni matukio yaliyogonga vichwa vya habari kama tulivyo yapokea katika chumba chetu cha habari leo jioni.
Mtoto aokolewa hai kutoka jumba lililoporomoka Huruma baada ya siku nne
Mtoto wa mwaka mmoja na nusu ameokolewa mapema hii leo kutoka vifusi vya jengo lililoanguka mtaani huruma jijini nairobi baada ya kuwa chini ya vifusi vya jengo hilo kwa siku nne.
Shirika la msalaba mwekundi nchini linasema mtoto huyo alipatikana akiwa amekalia karai lililokuwa limewekwa blanketi vizuri huku mwili wa mamake ukipatikana kando yake.
Viongozi mlima Elgon waafikiana kufanya kazi pamoja
Huku wengi wa wanasiasa nchini wakizidi kulumbana kuhusu uongozi, viongozi wa Mlima Elgon wameafikiana kufanyia kazi pamoja kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
Mbunge wa sasa wa Mlima Elgon John Bomet Serut kwenye hafla nyingi amesikika akikariri peupe kutokuwa na tofauti zozote za kibinafsi na mbunge wa zawani wa eneo hilo Fred Chesebe Kapondi akihoji kujitolea kwake kufanyia kazi pamoja na viongozi wengine.
Wakaazi Kanduyi waonywa dhidi ya pombe haramu
Wakaazi wa Matong’i na vitongoji vyake katika kaunti ndogo ya Kanduyi wameonywa dhidi ya ugemaji na uuzaji wa pombe haramu na badala yake kutakiwa kujihusisha na miradi itakayowafaidi kama jamii kwa ujumla
Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika kijijini humo O.C.P.D wa Bungoma David Kirui ameonya kwamba yeyote atakayepatikana akijihisisha na ugemaji na uuzaji wa
Usimamizi wa chuo cha anuai cha Matili kupigwa msasa
Mbunge wa Kimilili Suleiman Kasuti Murunga ameahidi kuwa usimamizi wa chuo cha anuai cha Matili utapigwa msasa kuhakikishachuo hicho kinawapa wanafunzi elimu bora baada ya sintofahamu kuzuka kufuatia kifo cha aliyekuwa mwalimu mkuu wa chuo hicho.
Murunga anahoji kuwa chuo hicho kina uwezo na vifaa vya kutosha kuwapa wanafunzi chuoni humo elimu bora akisema kama kiongozi amejitolea kuhakikisha wanafunzi wananufaika nacho
Viongozi wapinga shirika lisilo na misingi ya kidini kuhaliliswa
Viongozi wa makanisa katika kaunti ya Vihiga wamepinga hatua ya kuhalalishwa kwa shirika lolote lisilo na misingi ya kidini nchini huku wakitishia kufika mahakamani kupinga hatua hiyo.
Wakiongozwa na mwenye kiti wa viongozi wa makanisa katika eneo hili Isaac Wawire viongozi hao wamelalamikia hatua hiyo wakisema kuwa inaenda kinyume na sheria.
Taharuki yatanda nandi kufuatia mauaji
Hali ya taharuki imetanda katika kijiji cha Kapkures wilayani Nandi kusini baada ya mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 42 kupatikana amefariki baada ya kuawa kinyama na watu wasiojulikana asubuhi ya leo
Wakazi Pokot wahimizwa kuhama kuepuka mafuriko
Wakazi wanaoishi katika nyanda za chini katika kaunti ya Pokot magharibi wamehimizwa kuhamia sehemu ya miinuko ili kuzuia maafa yanayotokana na maporomoko ya ardhi msimu huu wa mvua.
Wakaazi Butere walalamikia barabara mbovu
Kufuatia mvua kubwa inayoendelea kushuhudiwa maeneo mengi ya humu nchini na
kusababisha maafa mengi, wakaazi pamoja na wahudumu wa bodaboda katika
wadi ya Marama kusini wilayani Butere, wamelalamikia hali mbovu ya barabara ya kutoka Manyala kuelekea Shiatsala.
Kwa kina cha habari hizi sikiliza West Fm katika masafa ya 94.9 na 104.1, au katika mtandao kwenye www.westfm.co.ke. Tegea runinga yetu ya West TV katika masafa ya Startimes 118 na Go Tv 805.