Yafuatayo ni matukio yaliyogonga vichwa vya habari kama tulivyo yapokea katika chumba chetu cha habari leo.
Viongozi wa matabaka mbali mbali na Wakenya wahudhuria mazishi ya mama Lucy Kibaki kumpa mkono wa Buriani katika mazishi yanayofanyika nyumbani kwake Othaya kaunti ya Nyeri.
Mwili wa marehemu mama Lucy Kibaki, aliyekuwa mke wa rais mstaafu Mwai Kibaki umesafirishwa kwa kutumia usafiri wa barabara jumamosi kutoka Nairobi hadi Othaya ambapo utazikwa rasmi na serikali.

Ibada ya mwisho ya mama Lucy itaandaliwa hadharani katika uwanja wa shule ya Othaya Approved na hatimaye mazishi yatakayoshuhudiwa na wageni waalikwa tu yaandaliwe katika shamba la Mwai Kibaki baadaye
Wakazi wa wadi ya Kinyoro waraiwa kuacha maandamano
Mwakilishi wa wadi ya Kinyoro Gilbert Kityo amewarai wakaazi wa wadi yake kuwa wavumilivu na kuachana na maandamano ambayo wamekuwa wakifanya wakilalamikia hali mbovu ya barabara akisema malalamishi hayo yanashughulikiwa.
Bunge la Kakamega lapitisha hoja
Bunge la kaunti ya Kakamega limepitisha hoja ambayo inapendekeza kubatilishwa kwa sheria za kuthibiti ukusanyaji wa pesa za kukarabati barabara kutoka kwa viwanda vya kusaga miwa vinavyohudumu katika eneo hilo.
Bungoma yatakiwa kufadhili dawa katika majosho Tongareni
Serikali ya kaunti ya Bungoma imetakiwa kufadhili uwepo wa dawa kwa majosho katika eneo bunge la Tongareni kusaidia wafugaji kukabiliana na swala la kupe wanaovamia mifugo wao.
Kwa kina cha habari hizi sikiliza West Fm katika masafa ya 94.9 na 104.1, au katika mtandao kwenye www.westfm.co.ke. Tegea runinga yetu ya West TV katika masafa ya Startimes 118 na Go Tv 805.